Nehemiah 3:3-8

3 aLango la Samaki lilijengwa upya na wana wa Hasenaa. Waliweka boriti zake, na wakaweka milango yake na makomeo na nondo. 4 bMeremothi mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, alikarabati sehemu iliyofuatia. Baada yake Meshulamu mwana wa Berekia, mwana wa Meshezabeli, alifanya ukarabati na aliyemfuatia ni Sadoki mwana wa Baana. 5 cSehemu iliyofuatia ilikarabatiwa na watu kutoka Tekoa, lakini wakuu wao walikataa kufanya kazi chini ya wasimamizi wao.

6 dLango la Yeshana lilikarabatiwa na Yoyada mwana wa Pasea, na Meshulamu mwana wa Besodeya. Waliweka boriti zake, na wakaweka milango, makomeo na nondo. 7 eKaribu nao ukarabati ulifanywa na watu kutoka Gibeoni na Mispa, yaani Melati Mgibeoni, na Yadoni Mmeronothi, sehemu hizi zikiwa chini ya mamlaka ya mtawala wa Ng’ambo ya Frati. 8 fUzieli mwana wa Harhaya, mmoja wa masonara, alikarabati sehemu iliyofuatia, naye Hanania mmoja wa watengenezaji marashi akakarabati sehemu iliyofuatia. Walitengeneza Yerusalemu mpaka kufikia Ukuta Mpana.
Copyright information for SwhKC